20 Apr 2021 / 160 views
Simba yaingia mkataba na Vunja Bei

Klabu ya Simba imeingia makubaliano ya kimkataba na mfanyabiashara maarufu nchini Fred Vunja Bei kwa ajili ya kuuza bidhaa za timu hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa mpango mkubwa wa timu hiyo ni kuendelea kutoa ajira kwa vijana kama ilivyokuwa sera ya Hayati, John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Awamu ya tano na sasa chini ya Samia Suluh ambaye anaendeleza kuiongza Tanzania baada ya Magufuli kutangulia mbele za haki.

Barbara amesema kuwa wengi waliomba tenda kwa ajili kuingia makubaliano na Simba ila mwisho wa siku wamempata Mtanzania, Vunja Bei.

“Ilikuwa ni wengi waliomba tenda ya kufanya kazi na Simba ila tunafurahi kusema kuwa Vunja Bei ambaye ni Mtanzania ameshinda tenda hiyo.

Atakuwa na kazi ya kusambaza bidhaa za Simba kila mahali nchini Tanzania na kutakuwa na mobile shop ambazo zitakuwa kila mahali, hata kwenye mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar pia atakuwa anasambaza bidhaa zetu.

  Vunjabei amesema kuwa anafurahi kufanya kazi na Simba na kupewa mamlaka ya kusambaza bidhaa hizo jambo ambalo atalifanya kwa uaminifu.